KITUO CHA MAFUNZO

Funguo zinazolifaa kusanyiko (people-compatible transpositions) ni kitu gani?

Umeisha jua kwamba Neo-Transposer inabadilisha ufunguo wa nyimbo kwa ajili ya sauti yako binafsi, au kwa maneno ya kitaalamu, voice range. Voice range maana yake nota zote ambazo unaweza kuziimba, kuanzia ile ya chini kabisa mpaka ya juu kabisa.

Hapo nyuma, ulipokuwa unaingia Neo-Transpose kwa kubadilisha ufunguo wa wimbo, programu ilikuonesha onyo ifuatayo:

Kumbuka: ufunguo huu ni bora kwa sauti yako binafsi, lakini inawezekana usiwafae watu wa kusanyiko kwa jumla.

...bila shaka, ukiwa umetumia Neo-Transposer kwa muda, utakuwa umegundua kuwa unapobadilisha ufunguo wa wimbo wo wote, wewe unafanikiwa kuuimba kwa urahisi, lakini watu wengine wa jumuiya wanapata shida kwa kuimba kiitikio, maana sauti yake inakuwa ya chini mno au ya juu mno. Haya yanatokea kwa sababu kila mtu ana voice range yake, sio kati ya wanawake na wanaume tu, bali wanaume kati yao na wanawake kati yao pia. Ndiyo maana inawezekana kwamba, baada ya kubadilisha nyimbo kadhaa, nazo ziwe rahisi kwako kuimba ila sio kwa watu wengine.

Sasa tufanye nini na tatizo hili? Inategemea na wimbo. Kwa nyimbo kadhaa haiwezekani kuoanisha voice range ya mwimbaji na ile ya kusanyiko. Kwa nyimbo zingine, Neo-Transposer imeendeleza Funguo zinazolifaa kusanyiko (people-compatible transpositions). Funguo hizi zinazingatia sio voice range ya wimbo na ya mwimbaji, bali pia zinazingatia voice range ya wimbo katika sehemu ambazo kusanyiko linaimba, na pia voice range ya kusanyiko. Kwa kulinganisha hizo voice range nne, Neo-Transposer inahesabu kordi ambazo zikiwa ndani ya voice range ya mwimbaji, zinafanya kiitikio kiwe ndani ya voice range ya kusanyiko.

El tono perfecto de un canto es, idealmente, la intersección etre el tono más cómodo para el cantor, el tono más cómodo para la asamblea y el tono que mejor refleja la intención del canto

Lakini ona, mahesabu haya ni kisio tu. Katika kusanyiko kila mmoja ana voice range yake, tofauti na ya mwenzake. Lakini kadiri ya uzoefu wangu kama mwimbaji, nimefafanua voice range ya kawaida (standard), ambayo nadhani watu wengi, waume kwa wake, wanaweza kuimba. Hii voice range ya kawaida (standard) ni kisio, isiyo kamili. Nayo ni B 2 → B 3, tukifikiri kuwa wanawake wataimba katika oktava moja juu ya wanaume, yaani B 3 → B 4).

Wakati Neo-Transposer inabadilisha ufunguo wa wimbo fulani kwa ajili ya sauti yako, hali moja kati ya hizi tatu tofauti inaweza kutokea:

1) Hali iliyo bora: ufunguo unaoifaa sauti yako tayari unaifaa sauti ya kawaida (standard) ya kusanyiko. Ikitokea hivyo, utaona onyo ifuatayo:

Kwa kordi hizi, hata watu wa kusanyiko wataweza kuimba wimbo huu kwa urahisi! Maelezo zaidi

2) Ufunguo unaoifaa sauti yako ni wa chini mno ama wa juu mno kwa kusanyiko. Ikitokea hivyo, Neo-Transposer itakuonyesha ufunguo mwingine, ambao utakuwa wa juu au wa chini zaidi kuliko ule uliokufaa wewe, ili uweze kulifaa kusanyiko pia. Ufunguo huu (ambao tunauita “unalifaa kusanyiko”) bado upo ndani ya voice range yako, yaani, bado unaweza kuimba, ijapo itakuwa ni ya chini au ya juu zaidi kuliko ule wa kwanza, unaohesabiwa bila kulizingatia kusanyiko. Ikitokea hivyo, Neo-Transposer itakuonyesha ifuatavyo:

Kordi hizi, ijapo chini kidogo, zinafaa kabisa sauti za watu wa kusanyiko.

3) Kuna nyimbo kadhaa ambazo voice range yake ni kubwa kuliko voice range ya kawaida (standard) ya kusanyiko. Maana yake, haiwezekani kamwe kusanyiko zima liweze kuimba kiitikio chote kwa urahisi.

Kordi hizi za juu zinakufaa wewe, lakini zinakuwa juu sana kwa watu wa kusanyiko. Zinazofuata zimeshushwa kidogo, ingawa kwa wengine bado zitakuwa juu.

Kuna mambo mengine mengi, lakini sio lengo la makala haya kuelezea michakato ya Neo-Transposer kwa ndani kabisa.

Kumbuka kwamba programu hii inakupa mapendekezo ya kisio, na haiaminiki 100%. Hata mimi binafsi mara kadhaa naimba nyimbo zingine kwa kordi tofauti na zile ambazo Neo-Transposer inanipa, kwa sababu mashine haiwezi kufanya kazi ya mwanadamu, angalau kazi hii. Unahitaji kufanya mazoezi ya kila ufunguo na kuona ikiwa inafaa ama la; au kuweka capo kwenye viumba vingine, nk. Na ukifanikiwa... bonyeza kwenye kitufe kijani (green button)!

Ukiwa na mashaka ama unataka kujua zaidi, unaweza kuniandikia barua pepe: [email protected].